← Rudi ARIA

Privacy Policy

Jinsi tunavyotumia taarifa zako

1. Taarifa tunazokusanya

Unapojaza fomu yetu ya quote, tunakusanya jina lako, jina la biashara yako, namba yako ya WhatsApp, aina ya biashara, idadi ya messages unazopata kwa wiki, na link ya social media au maelezo mafupi kuhusu biashara yako (ukipenda kutupa).

Pamoja na hayo, server yetu inarekodi taarifa za kiufundi kuhusu ziara yako. Tunazipanga katika makundi matatu:

Taarifa za kifaa chako: IP address, browser unayotumia, lugha ya browser, na aina ya kifaa (simu au computer).

Taarifa za eneo: country na city, zinazotokana na IP yako kupitia ipapi.co. Timezone pia.

Taarifa za matumizi ya page: muda uliokaa, scroll depth, referrer (umetoka wapi), UTM parameters kama zilipo, na unique visitor ID inayohifadhiwa kwenye cookie.

Tunakusanya hii ili kukuelewa vizuri kabla ya kukupigia. Call ikiwa ya maana tangu mwanzo, inakusaidia wewe zaidi ya sisi.

2. Kwa nini tunakusanya

Ku-qualify lead kabla ya call. Kabla hatujakupigia, tunataka kujua kama ARIA inakufaa au la. Hiyo inatuokoa muda wako na wetu.

Kuboresha landing page. Tunaangalia nini inafanya kazi na nini haifanyi kazi, ili tuendelee kuboresha ujumbe.

Kuwasiliana nawe kuhusu ARIA. Tukikupigia, ni kuhusu ARIA tu, si vitu vingine.

Hatutumii data yako kwenye matangazo ya wengine. Hatuuzi data yako kwa mtu yeyote.

3. Wapi tunahifadhi

Google Sheets (Google LLC). Lead zako zinahifadhiwa kwenye Google Sheet ya Zillim Digital. Google ndiye custodian wa server hizo.

Railway. Landing page yenyewe inashikiliwa kwenye server za Railway.

Plausible Analytics. Tunatumia Plausible kufuatilia pageviews tu. Plausible haina cookies, haina personal data, haina tracking ya cross-site.

ipapi.co. Tunapowasiliana na ipapi.co kupata country na city kutoka IP yako, ni request ya moja kwa moja, hatuhifadhi response yao popote isipokuwa kwenye sheet yetu.

4. Haki zako

Chini ya sheria ya Tanzania Personal Data Protection Act, 2022, una haki hizi:

Una haki ya kujua data gani tunayo kuhusu wewe. Una haki ya ku-request tu-delete data yako kabisa kwenye system zetu. Una haki ya ku-correct data yoyote isiyo sahihi.

Kwa request yoyote, andika zillimdigital@gmail.com au tuma WhatsApp +255 760 962 379. Tutajibu ndani ya masaa 72.

5. Cookies na tracking

Hatutumii cookies za third-party za matangazo. Tunatumia cookie moja tu inayoitwa visitor_id, inayotusaidia kujua kama umetembelea site kabla. Inakaa mwaka mmoja, na unaweza ku-delete wakati wowote kwenye browser settings yako. Plausible Analytics yenyewe haina cookies kabisa.

6. Mabadiliko ya sera hii

Tukiupdate sera hii, tuta-update tarehe chini ya page hii. Mabadiliko makubwa, tutawajulisha wateja wetu wa sasa kupitia WhatsApp au email.

Last updated: 2026-04-09