← Rudi ARIA

Terms

Sheria za kutumia ARIA

1. Kuhusu ARIA

ARIA ni AI agent platform iliyojengwa na Zillim Digital kwa ajili ya biashara za Tanzania. Tunajenga custom systems zinazounganisha WhatsApp, Google Sheets, na Google Calendar.

Kila biashara inapata system yake tofauti, iliyojengwa kwa products, lugha, na workflow yake. Si chatbot ya jumla. Si template.

2. Discovery call (50,000 TZS)

Kabla ya kujenga system yako, tunafanya discovery call ya dakika 30. Kazi yake ni kuelewa biashara yako vizuri, na kukuambia wazi kama ARIA inakufaa au la.

Gharama: 50,000 TZS, inalipwa kabla ya call. Malipo ni kupitia M-Pesa au Selcom Bank, namba: 0760962379, jina la mpokeaji: Elius Kamuhangire.

Baada ya kulipa, tuma screenshot ya transaction kwenye WhatsApp +255 760 962 379. Utapokea link ya Calendly ku-book saa ndani ya dakika 30.

Gharama hii inapunguzwa 100% kwenye setup fee yako ukiamua ku-sign up baada ya call. Yaani: 50,000 TZS unayolipa kwa call, inarudi kabisa kwenye fee ya setup.

Ukisiojitokeza kwenye call bila kutoa taarifa, haturudishi pesa. Ukihitaji kubadilisha muda wa call, tuambie angalau masaa 24 kabla, na tutapanga upya bila gharama.

3. Setup na monthly fees

Ukiamua ku-sign up baada ya discovery call, tunakubaliana kwenye tier inayokufaa: Starter, Growth, au Enterprise. Bei zote ziko wazi kwenye landing page.

Setup fee inalipwa mara moja kabla hatujaanza kujenga system yako. Monthly fee inalipwa kila mwezi, inakata siku ya kwanza ya kila mwezi. Ukiamua ku-cancel, toa notice ya siku 30. Hakuna penalty, hakuna long-term contract.

4. Dhamana

ARIA inafanya kazi kwa kutumia AI models za third party kama Anthropic na OpenAI. Hatuwezi kuhakikisha 100% uptime ya provider hizi, lakini tunafuatilia na kurekebisha matatizo haraka.

Tunahakikisha system yako inafanya kazi vizuri. Tatizo lolote, tuma WhatsApp, tunaangalia ndani ya masaa 24 za biashara.

Hatuwezi kuhakikisha matokeo ya biashara (sales, conversions, revenue, n.k.). Hiyo inategemea wewe, market yako, na product yako. ARIA ni chombo, si miujiza.

5. Data yako

Data yote ya customers wako inabaki kwako. Wewe unamiliki Google Sheet, sisi tunajenga tu system inayosoma na kuandika kwenye sheet yako. Hatuna access ya kuuza wala kushirikisha popote.

Ukiacha kutumia ARIA, tunakufutia workspace na disconnections zote ndani ya siku 7. Soma Privacy Policy kwa maelezo zaidi kuhusu data.

6. Sheria

Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatumika kwenye makubaliano haya. Ugomvi wowote utashughulikiwa na mahakama za Dar es Salaam.

Last updated: 2026-04-09